Sisi wataalamu wa Maabara tunapaswa kujifunza siku zote ili kuendana na mabadiliko ya dunia na teknolojia kwenye kada yetu. Pia tunakwenda kwenye zama ambazo cheti kitakuwepo tu kuonyesha umehitimu lakini ufanisi wa kazi yako ndio utakutambulisha. Nisiache kusema pia kuwa tuko kwenye zama ambazo tunashindana na maroboti kwenye fursa ambao wana ufanisi zaidi. Hivyo nikukaribishe kwenye Youtube chaneli yetu ili tuweze kujifunza kila siku na kupata taarifa mpya kila kuitwapo leo ili kujiweka bora kila siku. Ndio maana nakuomba usubscribe kwenye hii chaneli yetu ili tuweze kuwa wa kwanza kupata video zetu mara tu zinapotoka. Tusisahau kulike, kucomment na kushare kwa wengine ili kuungana mkono kwenye hii safari na kwa faida ya wengi zaidi. Hii ni 'Saniru TV, The Laboratory Medicine Academy. Grow Up In Laboratory Medicine'. Naitwa Saniru Bia Kimweri ni Mtaaluma wa Maabara Tiba (The Laboratory Medicine Academician).